دسترسی نامحدود
برای کاربرانی که ثبت نام کرده اند
برای ارتباط با ما می توانید از طریق شماره موبایل زیر از طریق تماس و پیامک با ما در ارتباط باشید
در صورت عدم پاسخ گویی از طریق پیامک با پشتیبان در ارتباط باشید
برای کاربرانی که ثبت نام کرده اند
درصورت عدم همخوانی توضیحات با کتاب
از ساعت 7 صبح تا 10 شب
ویرایش:
نویسندگان: MAWLÂNÂ BIYÂ’ AD-DÎN KHÂLID AL-BAGHDÂDÎ
سری:
ناشر: Hakikat Kitabevi Publications
سال نشر: 2016
تعداد صفحات: 112
زبان: Swahili
فرمت فایل : PDF (درصورت درخواست کاربر به PDF، EPUB یا AZW3 تبدیل می شود)
حجم فایل: 657 کیلوبایت
در صورت تبدیل فایل کتاب Imân na Uislam به فرمت های PDF، EPUB، AZW3، MOBI و یا DJVU می توانید به پشتیبان اطلاع دهید تا فایل مورد نظر را تبدیل نمایند.
توجه داشته باشید کتاب ایمان و اسلام نسخه زبان اصلی می باشد و کتاب ترجمه شده به فارسی نمی باشد. وبسایت اینترنشنال لایبرری ارائه دهنده کتاب های زبان اصلی می باشد و هیچ گونه کتاب ترجمه شده یا نوشته شده به فارسی را ارائه نمی دهد.
DIBAJI Tunanza kitabu na Basmala; jina lake Allah ndio lenye ulinzi bora Zawadi zake hazina kipimo; Ni mwengi wa rehema na Anapenda sana kuwaondolea waja madhambi na kuwasamehe. Allahu ta’ala watu wote waliopo ardhini anawafungulia milango ya kutafuta kile watakacho. Ameumba vitu venye faida na kuvituma au kuteremsha kwa kila mtu. Na Anawaongoza nakupata furaha ya kudumu. Na vile vile Anawaongoza Atakao kwenye njia sahihi miongoni mwa wale watu ambao waliacha njia sahihi (siaratwalmustakim) wakakufuru kwasababu ya kudanganywa na nafsi zao potofu au makundi mabaya au vitabu vyenye madhara makubwa au vyombo vya habari badae wakatubu. Na Anawaokoa kutoka kwenye kuangamia kwa milele. Hawateremshie neema Zake wale wenye jeuri ya kupindukia Anawaacha kuendelea kuishi ndani ya upotofu wanaopenda na kuridhia. Siku ya mwisho(kiyama) Atawasamehe wale Atakaopenda miongoni mwa waumini watakaokuwa wanafaa kuingi moto(jahannam) na Atawaingiza pepo(jana). Yeye pekee ndie muumbaji wakila kitu ambacho kina uhai, Allah Ndiye Anayelinda kila kitu kwa mda wote dhidi ya hofu na vitishio. Kwakujiamini wenyewe kwajina la Allahu ta’ala tukufu nakutegemea msaada kutoka Kwake tunanza kuandika kitabu hiki. Sifa njema ni zake Allahu ta’ala. Amani na baraka ziwe ju ya kipenzi chake Mtume Muhammad alaihi-s-salam. Na sala bora ziwendea watu wanyumba yake (Ahl al-Bayt) na juu ya wale wote ambao wameipigania dini hi kusonga mbele(maswahaba zake/ as- Sahabat al-kiram). Maelfu ya vitabu vyenye thamani vimeandikwa kuhusu mafundisho ya imani, yanayoamrishwa na yanayokatazwa na uislamu, na vingi miongoni mwa vitabu hivi vimetafusiriwa kwenye lugha tofauti tofauti za kigeni na kusambazwa kwa kila nchi. Kwa upande mwengine, watu wabaya(zindiki) ambao hawaoni mbali na – 5 – majasusi waingereza mara kwa mara wanashambulia faida za uislamu, ukarimu na mwanga wake yani yale yalioamrishwa na yale yaliokatazwa kwamba haya yanakiuka na haki za binadamu na kujaribu kuyafanyia mabadiliko pamoja na kudanganya waislamu. Hata hivyo, ni shukurani kwamba sasa hivi kila sehemu (nchi) wanavyuoni wakislamu wanafanya juhudi kubwa kueneza na kuulinda Uislamu. Wanavyuoni waislamu kwa kusikia kutoka kwa masahaba Mtume Sallallahu aleihi wa sallam watukufu walioandika vitabu wanaitwa (Wanaviuoni wa Ahli-i sunnat). Hotuba sizizofaa na makala kwa upande mwengine yameshuhudiwa ambayo yanatajwa kuwa yametolewa kwa kutumia Kur’an na hadith za mtume na kikundi cha watu ambao hawajapitia na kusoma vitabu vilivyoandikwa na wanaviuoni wa Ahl ssuna. Hali yakuwa hotuba hizi na makala haya yamethibishwa kuwa ye ufanisi usiofaa kwa ndugu zetu waislamu, ila yanawonyesha tu ujinga wa mawakala wake. Mtu yeyote anayedai kuwa Muislam au akaonekana anasali jamaa basi huyu mtu anafaa kutambulika kama Muislam. Badae akionekana kwenye mazungumzzo yake kwa mfano, mandishi yake au katika mwenendo wake ikitokea kitu ambacho kina hitilafu na mafunzo ya iman kama yalivyoelezewa na wanavyuoni wa Ahl as- Sunna, basi atambiwa kwamba anayoyafanya ni kinyume na Uislamu na asipoacha yatamfanya kuwa mpotofu au murtadi(mtu ambaye ametoka kwenye Uislamu baada yakua Muislamu). Na atambiwa ku yaacha kabisa na kutuubu. Na kama kwakutumia akili zake ndogo akapuuza yanayomwambiwa na kusema kwamba hataacha anayoyafanya basi huyu anafahamika kuwa ni mpotofu au murtadi. Hata akiendelea kusali sala (namaz) tanu kila siku, akaenda Makka na akafanya hijja na akaendelea kufanya ibada tofauti na kutenda mema hatoepuka janga hili hadi pale atakapoacha kufanya mambo hayo yanayomfanya mtu kafir na akafanya toba[1] hatokuwa Muislamu. Kwa kujifunza vizuri vitu ambavyo vinamfanya mtu – 6 – [1] Kufanya tauba ya madhambi maana yake ni kujuta kwakufanya dhambi, kisha ukamuomba Allahu ta’ala msamaha, kwamfano, kwakusema dua hi: “ Estaghfirullah al-adhim al-ladhi lailaha illa Anta Huwal hayy-ul-qayyum wa atubu ilaih” na kumuahidi Allah kutorejea kufanya madhambi tena. kafiri, ni jukumu la kila Muislamu kujikinga mwenyewe dhidi ya mambo yanayomtoa ndani ya Uislamu na kusababisha kuwa murtadi, na pia anapaswa kutambua vyema makafiri na waongo ambao wanajifanya kuwa Waislamu, hasa Majasus wauingereza na kukaa mbali na madhara yao. Rasulullah sall-Allahu ta’ala alaihi wa sallam alielezea katika hadith-i-sherif kwamba habari za uongo na zenye makosa zitatolewa ndani ya Kur’an al-karim na hadith-i-sherif nakusababisha makundi sabini na mbili(72) potofu kujitokeza. Hadith-i-sherif hi inafafanuliwa kwenye vitabu al-Beriqa na al- Hadiqa, ambavyo vilinukuu hadith-i-sherif hi kutoka kwenye vitabu viwill (2) maaruf Bukhari na Muslim. Hatupasui kuamini vitabu na mihadhara ya kikundi hiki ambao wanajitokeza kwa majina kama wanaviuoni wa kiislamu au profesa wa dini; na vilevile tunapasua kuwa uangalifu ili tusianguke kwenye mitego ya wezi wa dini na imani hawa. Zaidi ya hayo Waisilamu wasio nelimu au wenye elim ndogo, makominisit, mafreemasons pamoja na mamisionari wakikrisitu kwa upande mwengine maWahabi ambao wamepokea mafunzo kutoka kwenye wangereza na mayahudi, wanafanya jitihada kupoteza watoto wa Waisilamu kwa kufufua na kutumia mbinu mpya. Wafanya wawezalo ili kuteketeza au Kuangamiza Iman na Uislamu kwa kutumia makala yenye uongo, filamu, ukumbi wa michezo, radio na matangazo ya runinga pia mitandao ya kijami kama facebook, tweeter, whatsup, google, yahoo nakadhalika. Wantumia mamilion ya fedha kufanikisha lengo hili. Wanaviuon wakiislamu ‘rahimahumullah’ wamefanya jitihada kwa kuwajibu watu hawo na wamendelea kuonyesha njia ya Allahu ta’ala ambayo ni yenye furaha na uokovu. Miongoni mwa hao, tumechagua kitabu kinachoitwa I’tiqad-nama kilichoandikwa na Mawlana Diya’ad-din Khalid al-Bagdadi al-Uthmani ‘quddisa sirruh; ambaye nu mwanachiuoni maarufu. I’tikad-nama ni kitabu kilichotafusiriwa kwa lugha ya kituruki na marehem Haji Faizullah Efendi mkaazi wa Kemah, Erzinjan, nakupewa jina Faraid al-fawaid na kuchapishwa mwaka 1312 A.H Egypt. Tafsiiri hi imerahisishwa kwa jina Iman na Uislamu. Toleo lake lakwanza ni mwaka 1966. Maelezo yetu yamewekwa kwenye mabano ( ). Tunamshukur Allahu ta’ala kwa Kutujaalia kuweza kuchapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili na – 7 – kwa mara ya kwanza. Asili ya kitabu hiki I’tikad-nama, ni lugha ya kifaaris na bado ipo kwenye maktab ya chuo cha Istanbul (Idara ya Ibnul Emin Mahmud Kemak, nambari F. 2639). Tafsiir yake ya Kituruki ilichapiswa na Hakikat Kitabevi) kwa jina la (Iman ve Islam). Katika kitabu (Durr-ul-muhtar) kilichoandikwa na mwanaciuoni mukubwa Alauddin-i Haskefi “rahimahullahu ta’ala”, mwisho wa mlango wa ndoa ya kafir anaelezea kwamba, “ binti wa kiislamu alieolewa au kuposwa halafu akabalehe au kutimza miaka ya uzima na akawa hajuyi nguzo za iman na hajitambui kama ni muislamu basi ndoa yake inakuwa batili (anakuwa murtadi). Anapaswa kufundishwa majina ya Allahu ta’ala na anafaa kuyarudia na kusema na’amini haya. Kufafanuwa haya, mwanachouin Ibn Ab’d’n rahmahullah ta’al alisema; mtoto wa kike anapokuwa mdogo, hufuata itikadi ya wazazi wake; na anakuwa Muislamu. Lakini anapokuwa (kubalehe) hafati tena itikadi ua wazazi wake kwasababu anajamulia mwenyewe. Anapotimiza umri wa utu uzima (kubalehe) na akawa hana elimu kuhusu Uislamu na hajitambui kuwa Muislamu basi anakuwa murtadi. Akijifunza nguzo sita za Iman bila kuamini na asipojua umuhimu wa Uislamu, basi hata akitamka kalimatu tauhid (akitoa shahada) yani Lailaha illallah Muhammad rasulullah hawezi kuendelea kama Muislamu. Anafaa kufahamu mambo sita ndani ya (Amantu billah...) piaamri zake Allahu ta’ala na Aliokataza kuyakubali na kuyatekeleza. Ibn Abidin katika uchambuzi hu anaonyesha kwamba mtu kafir akisema kalimatu ttauhid na akamini maana yake basi mda huo anakuwa Muislamu. Lakini kama waislamu wengine akipata nafasi anafaa kukariri maneno yafatayo pamoja na maana yake: “Amantu bi’llahi wa Mala’ikatihi wa Kutubihi wa Rusulihi wal-yawm-il-akhiri wa bil-qadari khairihi wa sharrihi minallahi ta’ala walba’thu ba’dal maut haqqun ash-hadu an la ilaha illallah wa ash-hadu anna Muhammadan abduhu wa Rasuluhu.” Pia mtoto wa kiume (kijana) ambaye ni Muislamu asipojifunza nguzo sita hizi na akasema kwamba anazamini anakuwa murtadi anapofikisha umri wa watu wazima( kubalehe). Bada ya kujifunza nguzo hizi sita na kuzamini basi anakuwa amepata imani, bada ya hapo anawajibika kutafuta mafundisho ya kiislamu yote na kujielimisha, kwa mfano kujua amri – 8 – za Uislamu zinazoitwa farz na yaliokatazwa yanayoitwa haramu, jinsi ya kutia udhu, kuoga, sala inasiliwa vipi, mtu anasitiri vipi (awrat) utupu wake/sehemu za siri. Anapouliza mtu kuhusu mafunzo haya basi ni lazima kwa yule alieuilwa kumfundisha au kumuelekeze kitabu sahihi kitakachomsaidia kupata maelezo hayo. Akikosa kupata kitabu au mwalimu basi ni lazima atafute mmoja au kitabu. Binti wa kike muislamu naye anawajibika kama anavyowajibika mtoto wa kiume. Basi pale anaposhindwa kutafuta mwalimu au kitabu kuhusu dini yake ya Uislamu anakuwa kafir. Atapata udhuru kwakutojua endapo atendelea kutafuta mwalimu au kitabu sahihi kya kiislamu asipotafuta basi anakuwa kafir moja kwa moja. Muislamu ambaye hatimizi farz (yale yalioamrishwa na Uislamu) kwa wakati wake au akatenda maovu(haramu) basi ataingizwa kenye moto jahanam. Kitabu hiki kya Iman na Uislamu kinaelezea kwa kina mafunzo kuhusu nguzo sita za iman. Basi kila Muislamu anapaswa kusoma kitabu hiki vizuri na afanye awezalo ili watoto wake na wale anowajua wapate kukisoma. Sehemu za awrat (utupu) zimefafanuliwa zaidi katika kitabu Endless Bliss juzu ya nne. Katika mandishi ya kitabu kiki maana ya ayet-i kerimas imeitwa ma’al inayomanisha ‘maana kama yalivyotolewa na wanaviuoni wa Tasfiir; kwani ayet-i karima au Kur’an maana yake aliifahamu Mtume Sall-Allahu alaihi wasala peke yake ; na halafu aliwafundisha masahaba zake. Wanaviuon wa tafsiir (ufafanuzi wa Qur’an al-karim) walitofautisha na kuchuja hadith zilizoletwa na wanafik na mazindiki ambao walipata mafunzo ya dini kutoka kwa Waingereza kama watu wasiofuata madhehebu ili waweze kuiharibu dini, na kuhusu zile hadith sherif wasizofahamu wanazitafsiir kulingana na maoni yao. Kinachofahamika na watu hao ambao hawajasoma dini ya Uislamu na wanasema kiarabu bila ilimu ya Tafsiir, basi ufafanuzi wao haujulikani kama tafsiir ya Qur’an tukuf. Ndio sababu hadith-i sherif inasema kwamba: ‘Mtu anayetafsir Qur’an karim(tukufu) kulingana na ufahamu wake basi anakuwa kafir.’ Kamusi ya kiarabu na maneno mengine yasiokuwa ya kingereza na ni mageni kwa msomaji wa kingereza yanaongezwa. Tunamuomba Allahu ta’ala Atuongoze kwenye njia sahihi ambayo ilionyeshwa na maulamaa wa Ahl as-Sunna! Tunamuomba – 9 – pia Atulinde dhidi ya kuamini uongo, udanganyifu na kuendelea kukubali uongo wa madui wa Uislamu wanaojiita la-madhab yani wasiokuwa na madhabu rasmi wanaotumia majina kama ‘ maulamaa wakuu wa Uislamu’! Vitabu vyote vinavyochapishwa kwenye lugha nyingi tofauti vinasambazwa ulimwengu kote kwa kutumia mtandao wa internet. KUMBUSHO: wa kristu wanajitahidi kuutangaza ukrisitu, Wayahudi nao wanajaribu kueneza Talmud, Hakikat Kitabevi wanafanya wawezalo kutangaza Uislamu na wa freemasons wanapigania kuhangamiza dini. Mtu mwenye akili, mwenye elimu na mwenye hoja atatumia mantik yake na kufanya chaguo sahih. Kwakutoa msada kwa kuenezaji wa njia sahih, itakuwa sabubu ya binadamu kupata furaha katika dunia hi na badae(Akhira). Ulimwengu wa Uislamu hivi sasa umegawanyika kwenye makundi makuu matatu. Kundi la kwanza ni Waislamu wa ukweli ambao wanafuata nyayo za ma Sahaba wa Mtume Sallallahu wa sallama. Na hao wanaitwa Ahl as-Sunna au Sunni Muslims au Firqa-i-naajiya, inayomanisha kundi ambalo limejiokoa kwenye moto. Kundi la pila ni madui wa masahaba, na hao wanaitwa Shi’i ( mashia) au Firqa-i-dalla (kundi lililopotea) . kundi la tatu linaitwa Wahhabi au Najid, mahali pa kuzaliwa kwao ni Najid Uarabuni. Na vilevile wanajulikana kama Firqa-i-mal’uuna (kundi lililola’niwa). Na katika kitabu chetu kinachoitwa Endless Bliss (Neema zisizo na mwisho) na The Rising and the Hereafter (Kufufuka na Kiyama) inaelezewa kwamba watu hawa wanaita Waislamu ‘makafir’. Na Mtume wetu Sallallahu aleih wasallama alilaani watu wanoita Waislamu vile. Uislamu kugawanyika kwenye makundi matatu haya ni natija/matokeo ya hila za Wayahudi na Waingereza. Kila Muislamu anapaswa kusema “La ilaha il-l-Allah,” mda wote ili kuitukuza nafsi yake, mfano kuitukuza nafsi yake kutokana na ujinga na maovu ambayo yanarithiwa na maumbile, na daima anafaa kurudia dua hi “Estaghfirullah,” ili autakase muoyo wake, mfano kuokoa moyo wake kutokana na ukafir na maovu ambayo yamefunika moyo wake kwa sababu ya nafsi yake kujingiza kwenya kundi la shetani na maovu, na katika kusoma vitabu hatari. Dua za watu wenye kuufuata Uislamu na kufanya tawba kwa makosa yao – 10 – waliofanya watakubaliwa na Allahu ta’ala. Mtu asiposali namazi(sala) tano kila siku, na akawatizama wanawake ambao hawajajifunika vizuri na wengine wanaonesha awrat( utupu) wao, na akala akanywa yale yalio haramu kula na kunywa, basi itahitimishwa kwamba mtu huyu hafuati Uislamu. Na dua zake hazitokubalika. Miladi Hijri Shamsi Hijri kamari 2001 1380 1422